Jumatatu, 30 Machi 2015

         SIRI NAMBA 1 YA MAFANIKIO: FANYA MAAMUZI YA WEWE KUWA MWANAMAFANIKIO. Ili uweze kufikia mafanikio kitu cha kwanza amua kuwa mwanamafanikio na jiwekee malengo na mipango nini unataka kufanya na kwanini umeamua. kufanya kitu chochote katika maisha ni lazima kwanza wewe mwenyewe uamue ukishafanya hivyo akili yako itakuwa inafanya kazi kulingana na wewe unavyoituma.
Ukiamua kufanya jambo anza SASA kwani kesho huanza leo na kesho haipo tabia ya kuhairisha mambo kila siku ndio chanzo cha wewe kutofikia malengo yako. Amua leo ili uweze kuona mafanikio badaye unapoendelea kusubiri ndivyo muda na umri unazidi kwenda usisubiri hali ya ukamilifu katika maisha ukisema hivyo utakuwa unajidanganya  binadamu mwenyewe hajakamilika.