Jumamosi, 23 Mei 2015

Haya ndio matumizi mazuri ya mshahara wako ambayo yatakuletea mafanikio

GAWANYA MSHAHARA WAKO KATIKA BAHASHA HIZI TANO
Mshahara ni makubaliano ya malipo kati ya mwajiri na mwajira kulingana na kazi anayofanya mwajiriwa kwa muda  au kipindi fulani kutokana na mkataba wao waliojiwekea waweza kuwa mwezi.
Wakati mwingine unafanya kazi na kupata mshahara lakini hujui au hufahamu sehemu au makundi unayoweza kuugawa mshahara wako.
Zifuatazo ni bahasha tano ambazo unaweza kuugawa mshahara
  1. SADAKA(Tithe Fund)
Unapopata mshahara wako asilimia kumi ya kipato chako  yaani mshahara weka katika bahasha hii au mfuko huu wa sadaka. Kutoa asilimia kumi ya mshahara wako ni mwongozo wa kuufuata lakini siwezi kukulazimisha uamuzi uko mikononi mwako BO SANCHEZ katika kitabu chake cha My Maid Invest in the Stock Market alikuwa akiwaambiwa wafanyakazi wake yani wasaidizi wake hivi ‘’ You will grow in abundance think’’ usemi huu wa BO SANCHEZ una maanisha kuwa kuna faida sana pale unapotoa sadaka kama alivyonena hapo juu, ‘’ utakuwa katika uwezo mkubwa wa kufikiri’
  1. MATUMIZI ( Expense Fund)
Haya ni yale matumizi ya kila siku ya mahitaji ya nyumbani (daily needs) ambapo pia unaweza ukatenga fungu lingine la mshahara wako au kipato chako na kuweka katika bahasha hii ya matumizi.Hii itakusaidia sana kutotumia hela vibaya na kuwa na nidhamu ya pesa katika mshahara wako na itakusaidia kujuwa kwa mwezi matumizi yako yanagharimu kiasi gani.
  1. MSAADA ( Support Fund)
Katika jamii zetu kusaidiana ni jambo la kawaida msaada huo unaweza ukautoa kwa ndugu,jamaa,marafiki na nk.Pengine ni kumsaidia mtaji wa kuanzisha biashara au kuboresha biashara na mengine mengi kuhusiana na msaada.Hivyo weka sehemu ya mshahara wako katika bahasha hii ya msaada hii itakusidia kutoharibu bajeti zako nyingine.
  1. DHARURA (Emergence Fund)
Katika maisha yetu ya kibinadamu huwa tunapatwa na dharura sana,na ubaya wa dharura unakuja pale umepatwa na tatizo halafu huna hela ya haraka ya kutatua jambo hilo lakini kama ukiwa umeweka sehemu ya kipato chako katika bahasha hii wala hutopata shida ya kulitatua. Dharura ni nyingi katika maisha na zinatokea kwa ghafla bila taarifa kama vile ajali, radi au kifo kinavyotokea.ukiwa na hela ya dharura itakusaidia kuwa na amani ya akili (Peace of Mind).

  1. KUSTAAFU (Retirement Fund)
Hii ni njia moja nzuri ya kuweka akiba na kustaafu ukiwa milionea .Weka ,tenga akiba katika bahasha ya kustaafu na iwekeze hela hii katika soko la hisa . Hela hii weka katika bahasha ya kustaafu na usiitumie bali iwekeze katika soko la hisa na mwisho wa siku una staafu ukiwa milionea.
‘’Kila mtu ana matatizo yake ,Hakuna maisha yasiyo kuwa na matatizo ‘’ usemi huu umedhihirishwa katika kitabu cha Tough Times Never Last ,But Tough People Do kilichoandikwa na Robert H.Schuller’Everybody has problem. No life is problem-free’

          Asante kwa muda wako!

Jumatatu, 30 Machi 2015

         SIRI NAMBA 1 YA MAFANIKIO: FANYA MAAMUZI YA WEWE KUWA MWANAMAFANIKIO. Ili uweze kufikia mafanikio kitu cha kwanza amua kuwa mwanamafanikio na jiwekee malengo na mipango nini unataka kufanya na kwanini umeamua. kufanya kitu chochote katika maisha ni lazima kwanza wewe mwenyewe uamue ukishafanya hivyo akili yako itakuwa inafanya kazi kulingana na wewe unavyoituma.
Ukiamua kufanya jambo anza SASA kwani kesho huanza leo na kesho haipo tabia ya kuhairisha mambo kila siku ndio chanzo cha wewe kutofikia malengo yako. Amua leo ili uweze kuona mafanikio badaye unapoendelea kusubiri ndivyo muda na umri unazidi kwenda usisubiri hali ya ukamilifu katika maisha ukisema hivyo utakuwa unajidanganya  binadamu mwenyewe hajakamilika.