GAWANYA MSHAHARA WAKO KATIKA BAHASHA HIZI TANO
Mshahara ni
makubaliano ya malipo kati ya mwajiri na mwajira kulingana na kazi anayofanya mwajiriwa
kwa muda au kipindi fulani kutokana na
mkataba wao waliojiwekea waweza kuwa mwezi.
Wakati mwingine unafanya kazi na kupata mshahara
lakini hujui au hufahamu sehemu au makundi unayoweza kuugawa mshahara wako.
Zifuatazo ni bahasha tano ambazo unaweza kuugawa
mshahara
- SADAKA(Tithe
Fund)
Unapopata mshahara wako
asilimia kumi ya kipato chako yaani
mshahara weka katika bahasha hii au mfuko huu wa sadaka. Kutoa asilimia kumi ya
mshahara wako ni mwongozo wa kuufuata lakini siwezi kukulazimisha uamuzi uko
mikononi mwako BO SANCHEZ katika
kitabu chake cha My Maid Invest in the
Stock Market alikuwa akiwaambiwa wafanyakazi wake yani wasaidizi wake hivi
‘’ You
will grow in abundance think’’ usemi huu wa BO
SANCHEZ una maanisha kuwa kuna faida sana pale unapotoa sadaka kama alivyonena
hapo juu, ‘’ utakuwa katika uwezo mkubwa
wa kufikiri’
- MATUMIZI
( Expense Fund)
Haya ni yale matumizi
ya kila siku ya mahitaji ya nyumbani (daily needs) ambapo pia unaweza ukatenga
fungu lingine la mshahara wako au kipato chako na kuweka katika bahasha hii ya
matumizi.Hii itakusaidia sana kutotumia hela vibaya na kuwa na nidhamu ya pesa
katika mshahara wako na itakusaidia kujuwa kwa mwezi matumizi yako yanagharimu
kiasi gani.
- MSAADA
( Support Fund)
Katika jamii zetu
kusaidiana ni jambo la kawaida msaada huo unaweza ukautoa kwa
ndugu,jamaa,marafiki na nk.Pengine ni kumsaidia mtaji wa kuanzisha biashara au
kuboresha biashara na mengine mengi kuhusiana na msaada.Hivyo weka sehemu ya
mshahara wako katika bahasha hii ya msaada hii itakusidia kutoharibu bajeti
zako nyingine.
- DHARURA
(Emergence Fund)
Katika maisha yetu ya
kibinadamu huwa tunapatwa na dharura sana,na ubaya wa dharura unakuja pale
umepatwa na tatizo halafu huna hela ya haraka ya kutatua jambo hilo lakini kama
ukiwa umeweka sehemu ya kipato chako katika bahasha hii wala hutopata shida ya
kulitatua. Dharura ni nyingi katika maisha na zinatokea kwa ghafla bila taarifa
kama vile ajali, radi au kifo kinavyotokea.ukiwa na hela ya dharura itakusaidia
kuwa na amani ya akili (Peace of Mind).
- KUSTAAFU
(Retirement Fund)
Hii ni njia moja nzuri
ya kuweka akiba na kustaafu ukiwa milionea .Weka ,tenga akiba katika bahasha ya
kustaafu na iwekeze hela hii katika soko la hisa . Hela hii weka katika bahasha
ya kustaafu na usiitumie bali iwekeze katika soko la hisa na mwisho wa siku una
staafu ukiwa milionea.
‘’Kila
mtu ana matatizo yake ,Hakuna maisha yasiyo kuwa na matatizo
‘’ usemi huu umedhihirishwa katika kitabu cha Tough Times Never Last ,But Tough People Do kilichoandikwa na Robert H.Schuller ‘’Everybody
has problem. No life is problem-free’’
Asante kwa muda wako!